WHO yatambua juhudi za kutokomeza vikope Morocco

15 Novemba 2016

Shirika la afya ulimwenguni WHO leo limetambua juhudi kubwa za utokomezwaji wa ugonjwa wa vikope nchini Morocco ambao ulikuwa ni janga la kiafya la kijamii nchini humo.

Kwa mujibu wa taariafa WHO, takwimu za vikope ambao ni ugonjwa unaoongoza kwa kusababisha upofu duniani, unaoenezwa kwa kugusana macho na pua dhidi ya watu walioambukizwa husuani watoto, unaelezwa kuathiri watu katika nchi 42 na kusababisha upofu kwa watu karibu milioni mbili.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dr Margaret Chan, amenukuliwa akisema kuwa ni mafaniko makubwa kwa afya aya umma nchiniMorocco na kuongeza kuwa hilo limedhihirisha namna utashi wa kisiasa, elimu, ufuatiliaji na ujumuishwaji wa jamaii ulivyo muhimu na unavyoweza kusaidia katika kutokomeza magonwja

Miaka ya 1990 Morocco ilianza kutekeleza mkakati wa WHO unaojumuisha upasuaji wa macho yanayougua vikope,dawa za kuuwa vijiua vijasumu, usafishaji uso na kusafisha mazingira ili kuepuka maambukizi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter