Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yawekeza katika teknolojia kukwamua watoto

UNICEF yawekeza katika teknolojia kukwamua watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, leo limetangaza mpango mpya wa teknolojia unaoweza kusaidia kuimarisha maisha ya watoto hususani katika nchi zinazoendelea.

Katika mahojiano malum na idhaa hii  Meneja wa mfuko wa uvumbuzi katika UNICEF Bi Sunita Grote amesema shirika hilo linatumia njia ya teknolojia kusaka suluhu kwa changamoto zinazowakabili watoto mathalani katika elimu na afya ambapo shirika hilo linawekeza kufanikisha kupata takwimu, na kuwaunganisha watoto ili kutumia taarifa hizo katika kuwafikia .

Akifafanua  namna  mpango huu unavyosaidia jamii hasa watoto Bi Sunita anasema.

(SAUTI SUNITA)

"Mfano mwingine ni nchini Bangladesh, nchi hii inafanyia kazi mfumo wa kidijitali ambao utatumia komputa ndogo za kisasa au tablet ambazo zitatumiwa na wahudumu wa afya katika kukusanya taarifa. Watazunguka na vifaa hivi kuwasaka watoto ambao wameshapata chanjo au wanahitaji.