Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yazindua wiki ya kampeni ya uelimishaji kuhusu viuavijasumu

WHO yazindua wiki ya kampeni ya uelimishaji kuhusu viuavijasumu

Shirikia la afya duniani  WHO wiki hii linazindua kampeni kwa jina la “shughulikia kwa makini" au "Handle with care” ambayo ina lengo la uelimishaji wa viuavijasumu au antibayotiki.

Katika hafla maalumu ya uzinduzi wa kampeni hiyo mjini Beijing, China, mwakilishi wa WHO Dkt Bernhard Schwartländer ametoa wito kwa watu wote wakiwemo wataalamu wa masuala ya afya na watunga sera kote duniani ili kuzingatia umuhimu  wa madhara yatokanayo na dawa za viuavijasumu .

Katika wito wake Dkt. Schwartlander amesema usugu wa viuavijasumu unaweza  kumuathiri mtu yeyote  bila kujali umri  au jinsia.

Janga la usugu wa viuavijasumu tayari limesababisha vifo vya watu laki 7 duniani kote na wengi wao wakitoka katika nchi zinazoendelea.

Kwa mujibu wa utafiti wa WHO,  ifikapo mwaka 2050 wanakadiria vifo vya watu milioni 10 kutokana na usugu wa viuavijasumu .

China imekuwa mstari wa mbele katika kupambana na  tatizo la usugu wa viua vijiuasumu kwa kushirikiana na ofisi ya WHO nchini humo.