Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mitandao kunufaisha wafanyabiashara Kenya na Uganda

Mitandao kunufaisha wafanyabiashara Kenya na Uganda

Biashara zinazoendeshwa nchini Kenya na Uganda zitanufaika kufuatia uzinduzi wa mfumo mpya mtandaoni unaowezesha wafanyabiashara kuuza na kununua bidhaa kupitia mitandao.

Hii ni kwa mujibu wa habari kutoka kituo cha kimataifa cha biashara ITC ambacho kiko chini ya Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa mataifa, UNCTAD ambapo nchi hizi mbili zimezindua kitabu cha orodha cha intaneti.

Uzinduzi wa mfumo huo mpya mtandaoni kwa nchi hizi mbili utapitia kwa orodha ya "Wasafirihsaji nje wa Uganda" na "Wasafirishaji nje wa Kenya" zitawezesha makampuni katika kila nchi kuonyesha bidhaa na huduma zao kwenye intaneti na pia kuchapishwa katika magazeti ambapo makampuni ya kigeni yatapata fursa kuangalia huduma hizo na kununua bidhaa.

Mfumo huo mpya mtandaoni ulioanza operesheni mnamo tarehe 10 Novemba umepokea usaidizi wa kifedha kutoka kwa serikali ya Uholanzi. Ile orodha ya Uganda, mwenyeji wake itakuwa shirika la kitaifa la teknolojia ya habari (NITA-U), mwanachama wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia (ICT). Nayo nchini Kenya, mwenyeji wa orodha hiyo itakuwa shirika la kibinafsi la teknologia (KITOS).

Duru zinasema kipindi cha miaka mitano iliyopita, sekta ya teknologia ya Uganda imekuwa kwa kiwango cha wastani wa 19.7%, na kuongeza pato la taifa kwa 2.5%. Sekta hiyo huko Kenya imechangia kukua kwa uchumi na kuwapa kinachoitwa na kuongeza pato la taifa kwa karibu 25% ikiingiza dola bilioni 2 ifikapo mwaka wa 2017.

Mratibu, NITA Uganda Michael Newman Byamugisha amesema wao wanaendelea kuwezesha na kuboresha njia ya kufanya biashara na dunia kwa kupunguza changamoto za wakati na umbali kutoka kwa wanunuzi katika nchi nyingine za Afrika, Ulaya, Uingereza na Marekani. Naye Robert Skidmore, Mkuu wa Ofisi ya uendelevu ya ITC amesema hii itasaidia zaidi kuleta karibu soko la kimataifa na kuruhusu makampuni ya kigeni kuona huduma zinazotolewa katika nchi hizo mbili.