Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yafikisha msaada wa chakula kwa watu 100,000 Mosul

WFP yafikisha msaada wa chakula kwa watu 100,000 Mosul

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema limeweza kufikisha msaada wa chakula kwa watu zaidi ya 100,000 wanaokimbia mapigano huko Mosul, nchini Iraq.

Mwakilishi wa WFP nchini humo Sally Haydock amesema pamoja na kutoa msaada huo, bado wanaendelea kujitahidi ili wawafikie watu walionaswa katikati ya mapigano na kwenye maeneo mengine ambayo yamekombolewa.

Miongoni mwa waliopatiwa msaada ni watu Elfu 25 wakazi wa moja ya kitongoji mjini Mosul, ambacho kilikombolewa kutoka kwa waasi.

Kwa mwezi mmoja sasa, serikali ya Iraq na washirika wengine wa kijeshi wamekuwa wakipambana ili kuutwaa mji wa Mosul kutoka mikononi mwa magaidi wa ISIL au Da’esh.