Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Posta Afrika zaja na mbinu mpya za kimtandao kunufaisha wahamiaji na familia zao:IFAD

Posta Afrika zaja na mbinu mpya za kimtandao kunufaisha wahamiaji na familia zao:IFAD

Takwimu za karibuni kutoka taasisi ya kimataifa ya kilimo na maendeleo Afrika IFAD mjini Abidja, inasema Afrika imepiga hatua kubwa katika huduma za kimtandao za kutuma  fedha kupitia ofisi za posta. Huduma hizi nafuu  zikiwa ni njia kubwa za wahamiaji kutuma pesa kwa ndungu na familia zao vijijini zinajumulisha zaidi ya dola bilioni 65 za kimarekani mwaka 2015.

Bwana Pedro Pedro De Vasconcelos wa IFAD amesema ripoti hii mpya itawasilishwa  katika kikao cha taasisi ya kilimo na  maendeleo ya IFAD  kitakacho fanyika mnamo tatrehe 15 hadi 16 mwezi huu huko Abija , kwa lengo la kusaidia na kuendeleza huduma za posta katika miji na vijiji Afrika.