Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vitendo vya kigaidi vikome Beni:Baraza la Usalama

Vitendo vya kigaidi vikome Beni:Baraza la Usalama

Wajumbe wa baraza la usalama waliohitimisha ziara yao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wametoa wito wa kukomeshwa vitendo vya kigaidi vinavyoendelea mjini Beni Mashariki mwa nchi hiyo.

Ujumbe huo ulioon gozwa na balozi wa Angola na wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa uliwasili Beni Kivu ya Kaskazini Jumapili kutathimini hali ya usalama katika eneo hilo.

Watu wa eneo hilo wanakabiliwa na madhila kwa miaka mingi kutokana na machafuko yanayosababishwa na makundi yenye silaha ilikiwemo kundi la ADF kutoka Uganda.

Ujumbe huo umesisitiza haja ya kutekeleza mikakati imara kufurusha makundi hayo, ikiwemo pendekezo la kupeleka vikosi maalumu vitakavyoshirikiana na vikosi vya serikali ikiwemo jeshi na polisi. Naibu mwakilishi wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa ni Alexis Lamek

(SAUTI YA LAMERK)

"Kilicho dhahiri ni kwamba ili kutokomeza ADF ni lazima tushirikiane, wadau wote wanapaswa kuwa na jukumu, ndani ya MONUSCO na hata wa nje ya MOMUSCO. Tunazungumzia wadau wa kikanda lakini niongeze kwamba wananchi ni lazima wajumuishwe, washirikiane na MONUSCO, bila sh   ana na vikosi vya serikali. Ni muhimu sana kushirikiana kupambana na vikosi hivi vya kihalifu" 

Ujumbe huo leo uko Luanda Angola ambako unakutana na Rais wa nchi hiyo, Bunge na asasi za kiraia.