Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoendelea zashirikiana kukabili mabadiliko ya tabianchi-COP22

Nchi zinazoendelea zashirikiana kukabili mabadiliko ya tabianchi-COP22

Mkutano wa 22 wa mabadiliko ya tabianchi unaoendelea Marakech Morocco leo Jumatatu umeanza vikao vya ngazi ya juu, na moja ya mada ni ushirikiano wa Kusini-Kusini na mabadiliko ya tabianchi.

Kikao hicho kimeelezea jinsi gani ushirika wa Kusini-Kusini unavyoweza kuboresha uwezo wa nchi zinazoendelea katika kushughulikia changamoto za mabadiliko ya tabianchi, utekelezaji wa mkataba wa Paris na ufikiaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDGs.

Dr David Nabarro, ni mshauri maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030.

(SAUTI YA DR NABARRO)

“Ushirika wa Kusini-Kusini ni muhimu sana kwa sababu tunaona zaidi na zaidi nchi za Kusini zikijijengea utaalamu na matokeo ambayo wanabadilishana uzoefu na ni njia bora hususani kuzisaidia nchi zisizojiweza zilizo na matatizo mengi ya kukabiliana nayo, tunaamini kwamba tunapata matokeo mazuri.”