Skip to main content

Mkataba mpya unahakikisha nia ya pamoja ya amani Colombia: Ban

Mkataba mpya unahakikisha nia ya pamoja ya amani Colombia: Ban

Mkataba mpya wa Amani baina ya serikali ya Colombia na kundi la waasi la FARC unadhihirisha nia ya Amani ya nchi hiyo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa .

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili na msemaji wake, Ban Ki-moon amewapongeza Wacolombia kwa kusikilizana kwa wakati wote wa zoezi hili.

Kura ya maoni mapema mwezi Oktoba ilishinda dhidi ya mkataba wa kwanza wa kihistoria ulioafikiiwa baada ya miaka mine ya majadiliano baina ya pande hizo mbili.

Mkataba mpya uliokarabatiwa unajumuisha mapendekezo ya makundi yanayowakilisha Wacolombia waliopiga kura ya hapana kwenye kura ya maoni ya Oktoba pili.

Kwa mujibu wa habari mkatab huo mpya hautopigiwa kura ya maoni. Ban amewashukuru wote waliohusika kuja na mapendekezo ya kurekebisha mkataba huo na kusema Wacolombia sasa wana fursa ya kusonga mbele kuelekea njia ya amani wakiwa wana umoja kuliko wakati mwingine wowote.

Ban Ki-moon pia amezipongeza pande zote kwa kushikilia msimamo wa usitishaji uhasama na vitendo vua ukatili.