Viongozi wa Somalia wajadili muafaka wa usitishaji uhasama Gaalkacyo:

Viongozi wa Somalia wajadili muafaka wa usitishaji uhasama Gaalkacyo:

Viongozi wa Somalia wakiongozwa na waziri mkuu Sharmarke na washirika wa kimataifa wamehudhuria mkutano wa muafaka wa usitishaji uhasama Gaalkacyo na kuafikiana njia ya kusonga mbele katika kutatua mzozo.

Rais Abdiweli Mohamed Ali Gaas wa Puntland na Rais Abdikarim Hussein Guled wa Galmudug nao wamehudhria mkutano huo ili kujidhatiti na usitishaji uhasama kwenye mji huo wenye mzozo chini ya uongozi wa waziri mkuu Omar Abdirashid Ali Sharmarke wa serikali ya shirikisho ya Somalia.

Mwwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating, ndiye aliyeoongoza ujumbe wa washirika wa kimataifa uliojumuisha balozi wa Muungano wa Ulaya Somalia Veronique Lorenzo, Jenerali Gebre wa IGAD na naibu mwakilishi maalumu wa Kamisheni ya mwenyekiti wa Muungano wa Afrika Lydia Wanyoto.

Mapigano ya Gaalkacyo yamekatili maisha ya watu 45 katika wiki sita zilizopita na kuwaacha watu wengine 90,000 wakizihama nyumba zao kufuatia machafuko hayo. Keating amesema huo ulikuwa mkutano muhimu na Umoja wa Mataifa na wadau wa kimataifa wataunga mkono muafaka na mipango mingine ya kusitisha machafuko mara moja na kusiswtiza kuwa ukiukwaji wa makubaliano haukubaliki na watakaohusika na ukiukwaji huo watawajibishwa.