Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio la kigaidi Pakistan:

Ban alaani shambulio la kigaidi Pakistan:

Shambulio la kigaidi dhidi ya waumini kwenye hekalu la Sufi Kusini Magharibi mwa Pakistan limelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa duru za habari mlipuko mkubwa wa bomu kwenye hekalu hilo umekatili maisha ya watu 52 na kujeruhi wengine 100. Sherehe ya kidini ilikuwa ikifanyika wakati bomu hilo liliolipuka wilayani Kunduz jimbo la Baluchistan.Kundi la kigaidi la ISIL limeripotiwa kudai kuhusika na shambulio hilo.

Ban ametoa wito kwa serikali ya Pakistan kuwafikisha wahusika kwenye miono wa sharia , n pia ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga na kuwatakia ahuweni ya haraka majeruhi.