Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DRC : Baraza la usalama lahakikishiwa majadiliano zaidi Kinshasa

DRC : Baraza la usalama lahakikishiwa majadiliano zaidi Kinshasa

Ujumbe wa baraza la Usalama la Umoja wa mataifa uliokuwa ziarani Kinshasa nchini Jamhuri nya Kidemokrasia ya Congo DRC, umeondoka mjini humo kuelekea Mashariki mwa nchin kwenye mji wa Beni ukiwa na hakikisho la kuendelea kwa mjadala wa kisiasa wa taifa hilo.

Hayo ni kwa mujibu wa balozi wa Angola kwenye Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa ujumbe huo wakati wakifanya mkutano wa waandishi wa habari.

Wajumbe hao 15 wa baraza la usalama wamekutana wa nawadau wote nchini DRC Jumamosi akiwemo Rais Kabila, waziri mkuu, bunge, ujumbe wa upinzani na asasi za kiraia.

Balozi Ismael Abraao Gaspar Martins amesea ujumbe wa bgaraza umukwenda DRC kuchagiza diplomasia badaa ya kuzuka tafrani uchaguzi ulipoahirishw, ameongeza kuwa ziara hii liufanya ujumbe huo kuondoa mashaka waliyokuwa nayo

(SAUTI GASPAR MARTINS)

"Lazima niseme kwamba wajumbe wote 15 wa baraza la usalama wameungana kwa kauali moja kuhusu hitimisho hili, mashaka tuliyokuwa nayo yamepungua, na hakikisho tulilokuwa tunalitafuta nadhani tunalipata, kwasababu kila mtu ana utashi wa kuepuka zahma”

Naye balozi wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Francois Delattre,ambaye pia ni nmwenyekiti wenza wa ujumbe huo amesema huu huenda ukawa wakati wa kihistoria kwa DRC, kwani nchi hiyo inaweza kushuhudia kipindi cha mpito cha uongozi kwa Amani baada ya Rais kumaliza muda wake, na itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo. A amekaribisha hatua hiyo na kusema

(SAUTI DELATTRE)

"Kwanza wote kupiga machafuko na kuchagiza majadiloiano, huo ndio msingi wa kila kitu na naamini kwamba ni suala linalowaleta pamoja wadau wote tuliokutana nao, pili ni kusaka suluhu ya kisiasa kwa misingi ya kuheshimu katiba, naamini hili ni muhimu na pia ni kipengee kinachowaleta pamoja wadau wote tuliokutana nao, na tatu uelewa mpana kwa misingi ya kikanda na kimataifa , wadau tuliokutana nao wanakumbuka jinsi DRC inavyozungukwa na majirani tisa na kuifanya kuwa nchi yenye majirani wengi Afrika. Na wote wanatambu kwamba kinachotokea katika nchi hii kina athiri hali ya kanda nzima”

Wajumbe hao sasa wameelekea Beni kabla ya Jumatatu kuondoka kwendaLuanga Angola.