Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumza na Rais Trump kwa simu:

Ban azungumza na Rais Trump kwa simu:

[caption id="attachment_300955" align="alignleft" width="300"]bantrump

Katika mazungumzo kwa njia ya simu Ijumaa , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amempongeza Bwana Donald Trump kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa 45 wa Marekani.

Kupitia taarifa ya msemaji wake Ban amekaribisha wito wa Rais huyo mteule wa kurejesha Umoja nchini Marekani baada ya kampeni ngumu ya uchaguzi iliyoghubikwa na mambo mengi.

Katibu Mkuu pia ameelezea imani kwamba Marekani na Umoja wa Mataifa watadumisha utamaduni wa ushirika imara ili kupiga hatua katika masuala ya amani na usalama, maendeleo endelevu na haki za binadamu kote duniani.

Wawili hao wameaafikiana kuendelea kuwasiliana.