Skip to main content

Haki izingatiwe dhidi ya madhila kwa raia Iraq: Zeid

Haki izingatiwe dhidi ya madhila kwa raia Iraq: Zeid

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra 'ad Al Hussein ametoa wito leo wa hatua za haraka kuchukuliwa ili kuhakikisha kwamba haki na mahitaji ya waathirika vinazingatiwa ikiwa ni pamoja na kuangalia kiundani, haja ya haki, ukweli na maridhiano nchini Iraq.

Ofisi yake imepokea habari kuhusu makaburi ya pamoja, ushahidi zaidi wa vitendo vya ukatili wa kingono kwa wanawake na wasichana, mateso na mauaji, ajira kwa watoto na ukiukwaji mwingine mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na ISIL nchini Iraq.

Amesema kuna ripoti iliyoibuka ya visa mbalimbali vya mateso dhidi ya raia, akiongeza kuwa picha zinazoonekana ni za kusikitisha mno, watoto wana lazimishwa kufanya mauaji, wanawake kugawanywa miongoni mwa wapiganaji wa kigaidi wa ISIL na mauaji ya wale wanaodhaniwa kwenda kinyume na mafundishoya ISIL. Amesema maelfu ya raia ni wakimbizi wa ndani ambapo wanatumika pia kama ngao ya wakati wa vita.

Ameiomba serikali ya Iraq kurejesha utekelezaji madhubuti wa sheria haraka katika maeneo waliyokomboa ili kupunguza mashambulizi ya kulipiza kisasi pamoja na adhabu.