Wahamiaji kutoka pembe ya Afrika warejea nyumbani kwa msaada wa IOM
Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanza tena operesheni za kuwawahamisha wahamiaji waliokwama nchini Yemen baada ya kusita kwa muda kufuatia mashambulizi ya anga na mapigano nchini humo. Rosemary Musumba na taarifa kamili.
(RIPOTI YA ROSEMARY)
Djibouti ambayo imekuwa ukipokea kundi kubwa la wahamiaji hao wengi kutoka Ethiopia na nchi zingine za Pembe ya Afrika wanaorejeshwa, inasema imezidiwa na sasa inahofia masuala ya afya na usalama wa wahamiaji hao wanaporejea.
IOM inasema mamia ya wahamiaji wamerejeshwa kwa nguvu wakiwa katika hali mbaya na hadi sasa wahamiaji 24 wamepoteza maisha Djibouti kutokana na mazingira waliorejeshwa kutoka Yemen ndio maana shirika hilo limeamua kuchukua hatua.
Kifikia sasa jumla ya wahamiaji 672 wamesaidiwa kuhamishwa kwa ushirikiano wa IOM Djibouti, Ethiopia na Yemen.