Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sukari na nafaka zachochea ongezeko la bei mwezi Oktoba

Sukari na nafaka zachochea ongezeko la bei mwezi Oktoba

Kipimo cha bei ya shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO kiliongezeka kwa pointi 172 mwezi uliopita, ikiwa ni ongezeko kwa asilimia 9.1 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya mwezi huu wa Oktoba iliyotolewa na FAO kupima wastani wa kiwango cha bei ya vyakula huku ikionyesha kuwa bei za nafaka zimeongezeka kwa mara ya kwanza ndani ya miezi mitatu .

Ongezeko hilo ni mwendelezo kwa mwaka huu wa 2016 isipokuwa mwezi Julai pekee ambapo bei ziliporomoka.

Kipimo hicho cha bei hufanyika kwa kufuatilia na kulinganisha bei za makundi makuu matano ya bidhaa muhimu zaidi duniani kwenye soko la kimataifa.

Bidhaa hizo ni pamoja na sukari, nafaka na zile zitokanazo na maziwa.

Dalili za mapema za makadirio ya 2017 inaonyesha majira ya baridi, kaskazini mwa Marekani kutasababisha wakulima kupunguza eneo la kilimo kwa sababu ya matarajio ya bei ya chini kwa mazao ya ngano kutokana na nguvu ya dola za Marekani.