Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukomboa Mosul kumeleta changamoto- Kubis

Kukomboa Mosul kumeleta changamoto- Kubis

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Jan Kubis amewasilisha ripoti yake kwenye Baraza la Usalama, akiipongeza serikali ya Iraq kwa ushirikiano wake, bila kusahau jeshi la usalama nchini humo linavyoendelea kukomboa mji wa Mosul na miji mingine.

Amesema ingawa hivyo, mapigano hayo yameleta changamoto nyingi na hofu kwa wakimbizi wa ndani na visa vya ukatili na mauaji dhidi ya raia vimeendelea kuripotiwa.

Bwana Kubis ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI amesema kwa sasa kuna wakimbizi zaidi 42,00 ambao wanahitaji msaada kwa haraka kutokana na mapambano hayo ya Mosul.

Amesema UNAMI na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa wametoa ombi la dola milioni 280 lakini kufikia Septemba ni nusu tu iliyopatikana.

Akimnukuu kiongozi mmoja wa Iraq Al Hakim Tal juu ya suala la demokrasia nchini humo, Bwana Kubis amesema..

(Sauti ya Kubis)

"Al Hakim Kal ametoa wito kuwepo kwa ushirikiano ambapo raia wote wanajihisi wanaweza kuchangia katika kukuza demokrasia. Na kwamba kugawanywa kwa nchi yao kukataliwe ili kuimarisha wajibu wa kikatiba.”