Vijana ni lazima wahusishe kupambana na mabadiliko ya tabia nchi:Al Hendawi

Vijana ni lazima wahusishe kupambana na mabadiliko ya tabia nchi:Al Hendawi

Vijana wana nguvu, uwezo wa kubadili mwelekeo wa mabadiliko ya tabia nchi endapo watashirikishwa katika vita hivyo. Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya vijana Ahmad Al Hendawi anayehudhuria mkutano unaoendelea wa mabadiliko ya tabia nchi mjini Marakech Morocco.

Mkutano huo leo umejikita kwenye kauli mbiu ya vijana na taifa la kesho kwa nia ya kusistiza mchango wa vijana katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s lakini pia kuchukua hatua dhidi ya changamoto za mabadiliko ya tabia nchi. Al Hendawi amesisitiza kwamba

(SAUTI YA AL HENDAWI )

Naamini kwamba ushishirikishwaji huo utaendelea kutoa msukumo na kuchagiza utekelezaji wa mkataba wa Paris na malengo ya maendeleo endelevu.”

Ameongeza kuwa vijana wakishirikishwa na wakiwezeshwa wanaweza

(SAUTI YA AL HENDAWI)

"Naamini vijana wana uwezo kama wapiga kura, wabunifu , kama wachagizaji katika jamii kuchukua hatua kuhusu tabia nchi leo na tunahitaji kuwaunga mkono."