Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama laridhia vikwazo dhidi ya Somalia na Eritrea.

Baraza la usalama laridhia vikwazo dhidi ya Somalia na Eritrea.

Baraza la usalama leo limepitisha azimio namba 2316 la vikwazo dhidi ya Somalia na Eritrea wakati huu ambapo taifa la Somalia lipo katika mchakato wa uchaguzi.

Baada ya kupitishwa kwa azimio hilo linalosongesha juhudi za kusaka amani katika ukanda wa pembe ya Afrika, mwakilishi wa kudumu wa wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa Balozi Mathew Rycroft amesema.

( SAUTI BALIOZI MATHEW)

‘‘Kupitishwa tena kwa azimio hili leo ni sehemu moja ya usaidizi wetu kwa Somalia, mchakato wa uchaguzi mwezi huu ni muhimu kwa mustakabali wa Somalia na tunatarajia kuisaidia serikali ya shirikisho hususani katika kuunda upya sekta ya ulinzi ambayo ni rahisi, inayowajibika, endelevu na inayokubalika kwa shirikisho  na mamlaka za kikanda.’’