Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waganda wandamana kupinga uchafuzi wa msitu Bugoma

Waganda wandamana kupinga uchafuzi wa msitu Bugoma

Wakati jumuiya ya kimataifa imefungua macho kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, watu zaidi ya elfu moja nchini Uganda, wameshiriki katika mandamano ya kupinga uharibifu wa msitu Bugoma magharibi mwa nchi hiyo. John Kibego na taarifa kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Wengi wao wakiwa walisafiri mwendo wa wa kilomita zaidi ya 150 hadi kwenye msitu huo, walihamasishwa na shirika la kutetea Wanyoro la BUKITAREPA.

Walijikita kambi katika kijiji cha Nsozi, karibu na eneo la msitu Bugoma linashindaniwa baina na Mamlaka ya Misitu NFA na ufalme wa Bunyoro Kitara kuanzia saa kumi na moja alfajiri.

Wanalaumu serikali kwa kushindwa kuzuia uharibifu wa msitu huo wa akiba.

Yusufu Bunya ni Msemaji wa BUKITAREPA.

(Sauti ya Bunya)

Mamlaka ya misitu imekanusha madai hayo. Naibu kamishina wa wilaya ya Hoima ni Ambrose Mwesigye.

(Sauti ya Mwesigye)

“Hamna vurugu. Lakini mandamano hayo hayakukubaliwa, hawana ridhaa waliyafanya kivyao. Tunatafuta njia ya kuyazima”

Ripoti ya mamlaka ya misitu inaonya kuwa ikiwa uharibifu w amisitu utaendelea kwa kasi ya sasa, Uganda haitakuwa na msitu wa asili mwaka 2020.