Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika yapiga hatua kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi-Ripoti

Afrika yapiga hatua kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi-Ripoti

Ripoti mpya ya benki ya dunia inaonyesha sha kuwa nchi za Afrika zinafanya vyema katika jitihada za kukabaliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Ikimulika muktadha huo kwa kuzingatia mkutano wa 22 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP22 unaoendelea mjini Marrakech Morocco, benki ya dunia imesema nchi kama vile Cote d’Ivoire na Nigeria zinatekeleza kwa mafanikio ikiwamo pia kupunguza hewa ukaa kwa mujibu wa mkakati wa Benki ya dunia.

Mpango huo uliopitishwa wakati wa mkutano wa 21 wa mabadiliko ya tabianchi nchini Ufaransa unalenga kuzisaidia nchi za Afrika kuepukana na madahra ya mabadiliko ya tabianchi.