Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa MONUSCO ajulia hali wahanga wa shambulio la Goma

Mkuu wa MONUSCO ajulia hali wahanga wa shambulio la Goma

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, Maman Sambo Sidikou ametembelea Goma, jimbo la Kivu Kaskazini kuwajulia hali majeruhi wa shambulio la Jumanne lililosababisha pia kifo cha mtoto mmoja.

Bwana Sidikou ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko DRC, MONUSCO aliambatana pia na mkuu wa vikosi vya ujumbe huo na balozi wa India nchini humo Ashok Warrier.

Watatu hao wakiwa na viongozi wengine walikwenda kwenye hospitali inayoendeshwa na MONUSCO ili kuwajulia hali majeruhi wakiwemo walinda amani kutoka India na ndipo Bwana Sidikou akasema..

(sauti ya Sidikou)

Shambulio hilo la jana lilitokea katika kitongoji cha Kyeshero na lililotokana na kilipuzi ambacho hadi sasa hakijafahamika.