Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumuishi na ushirikishi ndio ngao ya kukabili tabianchi- Morocco

Ujumuishi na ushirikishi ndio ngao ya kukabili tabianchi- Morocco

Mkutano wa 22 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, #COP22 ukiendelea huko , Marrakesh, Morocco, imeelezwa kuwa uwazi na ushirikishi katika mipango ya kudhibiti mabadiliko ya tabianchi ndio suluhu ya kukabili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mazingira wa ufalme wa Morocco, Dkt. Hakime El Haite akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa, wakati huu ambapo nchi yake ndio mwenyekiti wa mkutano huo.

Amezungumzia ushirikishi wa pande zote mathalani..

(Sauti ya El Haite cut 1)

"Kwa mara ya kwanza tumehusisha mashirika yasiyokuwa ya serikali ili wapaze sauti kwa kufanya kazi kwa pamoja na mataifa kwa masuala ya tabianchi.Tunahitaji kuwa na uwazi zaidi na kutengeneza mwongozo madhubuti utakaowahusisha serikali, makampuni ya kibinafsi katika kupunguzu utoaji wa hewa chafuzi ya ukaa ifikapo mwaka 2030.”