Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungmuzo jumuishi yatakiwa Burundi- UM

Mazungmuzo jumuishi yatakiwa Burundi- UM

Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu juhudi za kuzuia migogoro, Jamal Benomar, amesema kuna umuhimu wa kubaini haraka chanzo cha mzozo wa Burundi kwa kutumia mazungmuzo jumuishi na mchakato halisi wa kisiasa, unaoongozwa na serikali ya Burundi kama njia ya kuzuia madhara ya mzozo nchini humo. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Benomar amesema hayo katika taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa baada ya kuwasilisha kwenye kikao cha faragha cha Umoja huo siku ya Jumanne, taarifa kuhusu ziara zake ya hivi karibuni nchini Burundi na ukanda wa maziwa makuu.

Amesema kuna umuhimu wa mshikamano mpya baina ya serikali ya Burundi na Jamii ya Kimataifa, wote wakishiriki katika juhudi za kuimarisha amani na utengemano bila kuingilia uhuru wa Burundi.

Ziara hiyo ililenga kufuatilia utekelezwaji wa azimio la Baraza la Usalama nambari 2303 la mwezi Julai mwaka 2016, ambalo miongoni mwa mengine linataka kupelekwa nchini Burundi polisi kutoka Umoja wa Mataifa ili kufuatilia ukiukwaji wa haki za binadamu.