Skip to main content

Imani dhidi ya polisi imerejea Sudan Kusini: Munyambo

Imani dhidi ya polisi imerejea Sudan Kusini: Munyambo

Imani baina ya jamii na polisi nchini Sudan Kusini imerejea, miezi minne baada ya matukio ya kuuawa na kuporwa kwa raia katika vituo vya ulinzi vilivyo chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS, amesema kamishna wa polisi wa UNMISS Bruce Munyambo.

Katika mahojiano maaulm na idhaa hii kandoni mwa mkutano wa polisi wa Umoja wa Mataifa unaoendelea ikiwa ni sehemu ya matukio ya wiki ya polisi mjini New York, Munyambo amesema polisi wanatimiza wajibu wao.

( SAUTI MUNYAMBO)

Hata hivyo amesema polisi walinda amani wanakabiliwa na chnagamoto kadhaa ikiwemo idadi yao kutokidhi haja na miundombinu mibovu kama vile barabara.