Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa hauna waangalizi kwenye uchaguzi wa Marekani- Dujarric

Umoja wa Mataifa hauna waangalizi kwenye uchaguzi wa Marekani- Dujarric

Upigaji kura ukiwa unaendelea nchini Marekani, Umoja wa Mataifa umesema haujapeleka mwangalizi yeyote kwenye uchaguzi huo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric amesema hayo akizungumza na wanahabari mjini New  York, Marekani kufuatia madai ya kwamba chombo hicho kimesambaza waangalizi wa uchaguzi kufuatiatilia upigaji kura.

(Sauti ya Dujarric)

“Kwanza kabisa, ushiriki wa Umoja wa Mataifa kwenye chaguzi hutokana na ombi la nchi husika. na katika matukio mengi, Umoja wa Mataifa haujihusishi kwenye ufuatiliaji wa kura labda kwenye mazingira fulani. Huwa tunashiriki kwenye kuratibu waangalizi na kusaidia masuala ya vifaa. Lakini niweke wazi, hakuna waangalizi wa Umoja wa Mataifa kwenye uchaguzi wa Marekani  unaofanyika leo.”