Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tani zaidi ya bilioni moja za chakula hupotea kila mwaka-FAO/UNECE

Tani zaidi ya bilioni moja za chakula hupotea kila mwaka-FAO/UNECE

Takribani tani bilioni 1.3 cha chakula hupotea kila mwaka , huku watu wapatao bilioni moja wakikabiliwa na njaa kote ulimwenguni. Hayo ni kwa mujibu wa makadirio ya shirika la chakula na kilimo FAO na kamisheni ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya uchumi barani Ulaya UNECE.

Makadirio yao yanaashiria kwamba harasa za kiuchumi zitafikia dola bilioni 940 kwa mwaka kutokana na upotevu huo wa chakula, wakisisitiza kwamba endapo upotevu huo wa chakula ungekuwa nchi , basi utoaji wa hewa chafuzi ungeifanya nchi hiyo kuwa ya tatu duniani.

Kwa mujibu wa FAO/UNECE, kitendawili kikubwa ni kwa walaji, jinsi gani wanavyochagua vitu vya kununua ama la, ambayo ni sabababu kubwa ya upotevu wa chakula, na wengi wao imebainika hata hawaangalii tarehe za mwisho wa kutumia bidhaa wanunuazo na matokeo tyke nyingi huishia mapipani kama taka zilizloharibika.

Kutambua umuhimu wa walaji kulijua hilo sasa mashirika hayo yameandaa mkutano utakaofanyika Novemba 10 Geneva Uswis ukiwaleta pamoja wadau wa sekta ya chakula, wanaharakati, mashirika ya kimataifa na wataalamu wa masuala ya chakula , ili kubaini changamoto na maeneo muhimu ya kuyachukulia hatua kuzuia ongezeko la upotevu wa chakula.