Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udhibiti wa tumbaku; nchi zinazoendelea kupata usaidizi zaidi

Udhibiti wa tumbaku; nchi zinazoendelea kupata usaidizi zaidi

Mradi wa miaka mitano umeanzishwa ili kuwezesha nchi zinazoendelea kupata msaada wa dhati wa kutekeleza mfumo wa shirika la afya duniani, WHO wa mkataba wa kudhibiti tumbaku.

Sekretarieti ya mkataba huo imesema msaada huo utatoka Umoja wa Mataifa na wadau wake na unalenga kuwezesha nchi hizo kutekeleza vipengele vya mkataba huo ikiwemo kupiga marufuku matangazo ya bidhaa za tumbaku, kuweka maonyo ya hatari za kiafya kwenye bidhaa na kupiga marufuku uvutaji sigara kwenye maeneo ya umma.

Kupitia mradi huo, nchi za vipato vya kati na chini zitatangaziwa iwapo zinataka kujiunga mwaka huu kwani WHO inasema kuwa ifikapo mwaka 2030, asilimia 80 ya vifo vitokanavyo na matumizi ya tumbaku vitapatikana kwenye nchi hizo.

Nchi 179 pamoja na muungano wa Ulaya ni wanachama wa mkataba wa udhibiti wa tumbaku.