Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msalala yaonyesha njia katika ulinzi wa Albino Tanzania- UNESCO

Msalala yaonyesha njia katika ulinzi wa Albino Tanzania- UNESCO

Ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania umekuwa ni tatizo lililosababisha Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO kuchukua hatua. Hatua hizo zilihusisha mikakati ya kijamii yenye lengo la kushirikisha viongozi, jamii na watoa huduma kwa kundi hilo ili kupunguza na hatimaye kutokomeza ukatili huo ambao kati yam waka  2000 na 2015 umeshuhudia zaidi ya mashambulio 150 nchini humo. Je ni nini kilifanyika? Mathias Herman Luhanya ni afisa programu kutoka UNESCO na amezungumza na Assumpta Massoi wa Idhaa hii. Kwanza anaelezea msingi wa hatua hizo zilizofuatiwa na tathmini ambayo imewasilishwa leo mbele ya wadau huko Tanzania.