Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yalaani mashambulizi kwa kutumiwa kwa magari ya wagonjwa kama Iraq

WHO yalaani mashambulizi kwa kutumiwa kwa magari ya wagonjwa kama Iraq

Shirika la Afya duniani WHO limelaani mashambulizi ya kutumiwa kwa magari ya wagonjwa kama silaha kulenga raia kwenye miji ya Tikrit na Samarra nchini Iraq. WHO imepokea taarifa inaeleza kuwa wahanga waliendesha magari ya wagonjwa na kuua watu zaidi ya 20 na kujeruhi kadhaa zaidi katika eneo la kukagua barabara huko Tikrit na katika sehemu ya kuhifadhi magari mjini Samarra.

Taarifa hiyo imeongezea kuhusu matumizi ya magari ya wagonjwa kama silaha ikisema kuwa unatishia uwezo wa kutoa huduma za afya na za matibabu kwa haraka. Ikiwa magari haya yatashukiwa kama vitisho kwa uwezo wa usalama, uhuru wao wa huduma kwa wagonjwa na waliojeruhiwa upo hatarini kucheleweshwa na kutishia maisha.

WHO ina wasiwasi na vitisho vinavyoendelea kwa wafanyakazi wa afya na vifaa vya na usafiri. WHO inajaribu kujihusisha na mamlaka za kitaifa za afya na washirika ili kulinda wagonjwa, wafanyakazi wa afya, miundombinu ya afya na vifaa kutokana na vurugu kuweza kuwahudumia wote wanaohitaji huduma hizo.