Tukabiliane na ugaidi kisayansi: Eliasson

7 Novemba 2016

Lazima operesheni zetu za ulinzi wa amani zijielekeze katika makabiliano dhidi ya makundi yenye msimamo mkali na magaidi amesema Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson.

Akihutubia baraza la usalama katika mjadala wa wazi kuhusu amani ya kimataifa na usalama, Eliasson amesema katika maeneo mengi ambapo kuna machafuko makundi yenye misimamo mikali na ugaidi ni halisi na hivyo lazima kukabaliana nayo.

Amewaambia washirika wa mjadala huo kuwa mikakati ya hatua inapaswa kuwa mahiri na ya kina, nyumbulishi na mipango saidizi na kwamba.

(SAUTI ELIASSON)

‘‘Tutahitaji pia kurekebisha namna tunavyoendesha majukumu yetu ikiwamo ofisi zetu, kujengea uwezo, ushiriki wetu na jamii, na hatua endelevu.

Naibu Katibu Mkuu kadhdalika amesema uelewa mpana kuhusu mazingira ya maeneo ya operesheni za ulinzi awa amani, na kukuza uwezo wa uchambuzi vinahitajika.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter