Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukuaji wa teknolojia watishia matumizi ya silaha za kibailojia

Ukuaji wa teknolojia watishia matumizi ya silaha za kibailojia

Nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa kuhusu silaha za kibailojia wamenza mkutano wa kutathmini mkataba huo wakati huu ambapo maendeleo ya kisayansi na ongezeko la ukosefu wa utulivu wa kisiasa vinatishia usalama.

Mkutano huo unafanyika Geneva, Uswisi ambapo mkuu wa kitengo kinachosimamia utekelezaji wa mkataba huo kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa mjini humo Daniel Feakes amesema kumekuwepo na madai ya vitisho kutoka vikundi visivyo vya kiserikali kama vile ISIS.

(sauti ya Daniel)

“Kumekuwepo pia na uwezekano wa ongezeko la hatari ya makundi yasiyo ya kiserikali kupata na kutumia silaha za kibaiolojia.”

Wakosoaji wa mkataba huo wanadai kuwa hakuna mfumo wa kimataifa uliopo kuweza kufuatilia silaha hizo za kibaiolojia.

Kwa mantiki hiyo katika tathmini ya sasa nchi 170 wa mkataba huo ulioanza kutumika mwaka 1975 wanajadili.

Tathmini ya mwisho ilifanyika mwaka 2011.