Mkakati wa UNESCO waleta nuru kwa albino Tanzania

Mkakati wa UNESCO waleta nuru kwa albino Tanzania

Nchini Tanzania mkakati wa kijamii wa kukabili ukatili na ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi, au albino umeleta matumaini baada ya kutekelezwa kwa mwaka mmoja na nusu kwenye wilaya nne nchini humo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, liliandaa mpango huo ukihusisha wilaya za Misungi, Sengerema, Msalala na Bariadi ambapo mtafiti huru aliyefanyia tathmini amebaini mafanikio kama anavyoeleza Mathias Herman Luhanya, afisa programu kutoka UNESCO.

(Sauti ya Mathias)

Alipoulizwa iwapo mkakati huo uliohusisha elimu kwa viongozi, jamii na watoa huduma umepunguza mashambulizi na hata mauaji, Bwana Herman amesema..

(Sauti ya Mathias)