Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio dhidi ya MINUSMA, watatu wauawa, saba wajeruhiwa

Shambulio dhidi ya MINUSMA, watatu wauawa, saba wajeruhiwa

Shambulizi katika eneo la Mopti, kaskazini mwa Mali limesababisha vifo vya watu watatu wakiwemo raia wawili na mlinda amani mmoja huku watu wengine saba wamejeruhiwa.

Kufuatia tukio hilo la Jumapili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa taarifa akilaani huku akituma rambirambi kwa familia za wahanga, na wanachi wa Mali na Togo ambako ndio anatoka mlinda amani aliyeuawa.

Ban amewakatia ahueni majeruhi akirejela msimamo wa Umoja wa Mataifa kuwa mashambulio yanayolenga walinda amani yanaweza kuwa uhalifu wa kivita.

Amesisitiza kuwa mashambulizi hayo dhidi ya walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA hayatadhoofisha azma ya ujumbe huo ya kutekeleza kwa ukamilifu mamlaka yake ya kusaidia juhudi za serikali na pande husika kutekeleza mpango wa amani.

Katibu Mkuu amesisitiza ya kwamba jukumu la amani na usalama Mali ni la pande husika nchini humo na kwamba amezitaka kuendelea kushiriki kikamilifu kutekeleza mkataba huo wa amani.