Skip to main content

Ustawishaji wa miji Afrika Mashariki

Ustawishaji wa miji Afrika Mashariki

“Miji inaendelea kuwa makazi ya binadamu na ni kiini cha vitendo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, ukuaji wa dunia, amani na haki za bindamu.” Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwa siku ya miji duniani iliyoadhimishwa Oktoba 31 mwaka huu.

Yaelezwa kuwa ifiakapo mwaka 2050 idadi ya wakazi duniani itaongezeka kwa theluthi mbili.

Mwaka huu Umoja wa Mataifa umechagua kauli mbiu, “miji jumuishi, maendeleo kwa wote” kwa ajili ya kuhimiza mchango mkubwa wa ukuaji miji kama kitovu cha maendeleo ulimwenguni na ushrikishwaji wa jamii.

Barani Afrika miji inaendelea kukua huku watu wengi wakihama kutoka vijijini kuelekea mijini. Lakini je, hali ya miji hiyo ikoje? Tunaangazia Afrika Mashariki.