Skip to main content

Wahamiaji wa Niger waliokwama Libya warejea nyumbani

Wahamiaji wa Niger waliokwama Libya warejea nyumbani

Wiki hii shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM limewasaidia wahamiaji 167 raia wa Niger waliokuwa wamekwama kusini mwa Libya kurejea nyumbani.

Wahamiaji hao wanawake 48, watoto 40 na wanaume 79, wamesafirishwa kwa ndege maalumu iliyoandaliwa kwa ushirikiano na serikali ya Libya, ubalozi wa Niger mjini Tripoli, chama cha msalaba mwekundu cha Libya na ofisi ya IOM nchini humo.

Kwa mujibu wa IOM wahamiaji wote 167 wamewasili salama mjini Niamey, Niger.