Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu kuhusu Tsunami ni muhimu ili kupunguza athari- Ban

Elimu kuhusu Tsunami ni muhimu ili kupunguza athari- Ban

Kuelekea siku ya kimataifa ya kuhamasisha dunia kuhusu athari za Tsunami kesho Jumamosi, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema katika maadhimisho haya ya kwanza kabisa kufanyika, ni vyema kuweka mifumo ya kutoa onyo mapema ili kuepusha madhara.

Katika ujumbe wake amegusia mfumo wa kupashana habari wa zama za kale huko Japan ambapo kiongozi mmoja alitia moto shamba la mpunga ili kuepusha watu dhidi ya wimbi kubwa la Tsunami lililokuwa linakaribia ukanda wa Pwani.

Naye mwakilishi wa Japan kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Koro Bessho amezungumzia muziki unaochezwa kila saa Kumi na Moja jioni kupitia vipaza sauti vya umma kote nchini kwa lengo la kupashana habari....

(Sauti ya Koro Bessho)

“Ingawa unalenga kujulisha watoto warejee nyumbani giza limeingia, pia hutumika kukagua mifumo hiyo kama inafanya kazi kwa kuwa ndio hutumika kupeana habari au onyo la dharura na watu waweze kuhama haraka na kuepuka Tsunami kama ilivyofanyika huko Mashariki mwa Japan.”