Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapishi na mabadiliko ya tabianchi: #Recipe4Change

Mapishi na mabadiliko ya tabianchi: #Recipe4Change

Wakati leo mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi ukianza kutekelezwa rasmi , wapishi mashuhuri Joan, Josep na Jordi Roca wanaungana na mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo endelevu (SDG Fund) kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika mtazamo tofauti wa “upishi endelevu”

Katika miezi mitatu ijayo kaka hao watatu ndugu na mabalozi wema wa SDG Fund kwenye shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa maendeleo , waendesha mashindano ya upishi ambayo yatawaalika watumiaji wa mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram kuwasilisha dondoo za mapishi endelevu (#Recipe4Change).

Wamesema chakula hakipaswi kuwa tishio kwa maendeleo bali chanzo cha maendeleo endelevu. Kaka hao wamekuwa wakitumia mtazamo huko katika lengo lao la kupambana na umasikini na kuchagiza maendeleo endelevu, ukizingatia kwamba theluthi ya gesi chafuzi duniani inatokana na kilimo, kwa kuchukua mitazamo bora inayohusiana na uzalishaji wa chakula na matumizi yake kutakuwa na matokeo mazuri kwa afya na mazingira ya dunia.

Katika kila shindano atapatikana mshindi mmoja na hatimaye kupatikani mshindi wa jumla wa dunia ambaye atapata fursa ya kushiriki nsiku nzima kwenye mgahawa wa wapishi hao maarufu wa El Celler de Can Roca nchini Hispania na atapata fursa ya kupika chakula na kula nao.

Kaka hao wamesisitiza kuwa ili kufikia malengo ya SDG’s ni lazima kuwe na elimu na uelewa mkubwa wa jinsi gani chaguo la vyakula linaweza kuathiri afya na mazingira.