Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujumuisha utamaduni ni muhimu kukabili majanga Indonesia

Kujumuisha utamaduni ni muhimu kukabili majanga Indonesia

Kushirikisha jamii na kujumuisha utamaduni ni muhimu katika mkakati wa udhibiti wa majanga nchini Indonesia.

Hayo ni kwa mujibu wa Dian Triyansah Djani, mwakilishi wa kundumu wa Indonesia kwenye Umoja wa Mataifa, akizungumza Ijumaa kuhusu maadhimisho ya kwanza ya kisu ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu Tsunami.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba Indonesia ndiyo iliyoathirika vibaya zaidi wakati wa zahma ya Tsunami ya mwaka 2004 kwenye bahari ya Hindi. Zaidi ya watu 150, 000 walipoteza maisha.

Bwana Djani anaeleza njia wanazotumia kujiandaa hasa katika maeneo ya vijijini nchini Indonesiaq kuepusha janga kubwa

(SAUTI DJAN)

“Tunatumia utalaamu kama sms, tunatumia vyombo vya habari na tekinolojia nyingine, lakini pia kuishirikisha jamii katika kuunda mikakati ya kitamaduni, mfano tumeanzisha kitu kinaitwa kijiji kiimara, ambapo wanakijiji wanatumia ujuzi wao wa kitamaduni na elimu ya kujiandaa endapo janga litazuka”