Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo 725 zaidi Mediteranea mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana:IOM

Vifo 725 zaidi Mediteranea mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana:IOM

Inakadiriwa kwamba kumekuwa na vifo 725 zaidi vya wahamniaji waliojaribu kuvuka bahari ya Mediterranean mwaka huu ukilinganisha na kipindi cha kuanzia Januari hadi 4 Novemba mwaka 2015.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, linasema idadi hiyo ni baada ya wahamiaji wengine 240 kutoweka na kuhofiwa kufa maji baada ya boti mbili walizokuwa wakisafiria kuzama Jumatano wiki hii kwenye bahari ya Mediterranean kati ya Libya na Italia.

Ajali ya wiki hii imefanya idadi ya wahamiaji waliopoteza maisha mwaka 2016 kufikia 4,220, na kuufanya mwaka huu kuwa ndio mbaya zaidi kwa vifo vya wahamiaji baharini kuwahi kutokea katika historia.

Mwaka 2015 jumla ya wahamiaji na wakimbizi 3,770 walipoteza maisha wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean.