Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunachunguza kutoweka kwa Itai Dzamara:Zimbabwe

Tunachunguza kutoweka kwa Itai Dzamara:Zimbabwe

Hali ya haki za binadamu nchini Zimbabwe imemulikwa leo kwenye tathimini ya Umoja wa mataifa mjini Geneva. Taarifa ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi

(TAARIFA YA GRACE)

Katika tathimini hiyo serikali ya Zimbabwe imepata fursa ya kujibu kuhusu wasiwasi uliopo wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kubana uhuru wa kujieleza na utumuaji wa nguvu kupita kiasi unaofanywa na vyombo vya dola.

Hoja nyingine iliyopewa uzito ni habari za kutoweka kwa mwandishi wa habari Itai Dzamara, mjini Harare yapata miezi 18 iliyopita. Umoja wa mataifa umetoa wito kwa Zimbabwe kutekeleza wajibu wake wa kimataifa kwa kuheshimu katiba na hasa ulinzi kwa waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za binadamu. Akijibu hoja hiyo na hasa kutoweka kwa mwandishi wa habari Dzamara, makamu wa Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, amesema

(SAUTI MANANGWA-CUT 1)

“Katika kesi hii serikali inachunguza vyanzo vyote ili kubaini wapi alipo raia wetu, na kwa muktada huo serikali inashirikiana na familia ya mtu huyo aliyetoweka na wanash eria wa Zimbabwe wa haki za binadamu".