Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zaidi zahitajika kupunguza kiwango cha joto duniani- Ripoti

Hatua zaidi zahitajika kupunguza kiwango cha joto duniani- Ripoti

Ripoti mpya kuhusu utoaji wa hewa chafuzi duniani imetaka dunia ichukue hatua zaidi kupunguza utoaji wa gesi chafuzi zinazoharibu ukanda wa Ozoni. Amina Hassan na taarifa kamili.

(Taarifa ya Amina)

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP limesema katiaka ripoti hiyo ya leo kuwa utoaji wa gesi hizo chafuzi upunguzwe kwa robo zaidi ya kiwango kilichokuwa kimelengwa ifikapo mwaka 2030 iwapo ulimwengu unataka kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabianchi.

Ripoti hiyo imesema kiwango cha hewa ya ukaa mwaka 2030 kinatakadiriwa kufikia kati ya tani Bilioni 54 na 56, kiwango ambacho ni cha juu sana kuweza kudhibiti ongezeko la joto lisifikie nyuzijoto mbili katika kipimo cha selsiyasi.

Kwa mantiki hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa UNEP Erik Solheim amesema mkataba wa Paris na hata makubaliano ya Kigali yanaonyesha njia, lakini ni vyema kuchukua hatua zaidi kwenye nishati endelevu, mathalani usafiri usiochafua mazingira, hatua ambazo amesema zihusishe kwa pamoja sekta ya umma na ile binafsi.