Mashauriano Burundi, Mkapa kuimarisha mawasiliano na wadau

2 Novemba 2016

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Said Djinnit amesema jitihada za kina zinaendelea kuchukuliwa ili kufanikisha mashauriano ya dhati baina ya wadau wa kisiasa nchini humo.

Bwana Djinnit amesema hayo Jumatano mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati akiwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu utekelezaji wa mkataba wa amani, ulinzi, usalama na ushirikiano huko DRC na ukanda wa Maziwa makuu.

Amesema tayari amekuwa na mazungumzo na msuluhishi wa mzozo wa Burundi, Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa ambapo amemsihi aendelee na jitihada za kuweka mazingira bora ya mazungumzo ya pamoja chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,EAC.

(Sauti ya Djinnit)

“Napenda kueleza kuwa msuluhishi anania ya kuimarisha mawasiliano rasmi na yasiyo rasmi na wadau wa Burundi na viongozi kwenye ukanda huo. Halikadhalika natia moyo juhudi za EAC kwa kuzingatia mkutano wangu na Rais Yoweri Museveni wa Uganda tarehe 19 mwezi Oktoba.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter