Skip to main content

UNHCR yahitaji dola milioni 60 kusaidia wakimbizi wa ndani Mosoul wakati wa baridi

UNHCR yahitaji dola milioni 60 kusaidia wakimbizi wa ndani Mosoul wakati wa baridi

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wiki hii limeanza kugawa msaada wa vifaa muhimu vya kujikimu kwa baridi kwa wakimbizi wa ndani milioni 1.2 nchini Iraq, pamoja na familia zilizotawanywa hivi karibuni na operesheni ya kijeshi inayoendelea Mosoul.

Watu wengine wanaohitaji msaada huo ni familia zinazohifadhi wakimbizi hao kote Iraq. Jumla ya wakimbizi 178,000 wa Syria watafaidika na msaada huo.

Ugawaji wa msaada huo umeanza licha ya mpango wa msaada wa baridi wa UNHCR ambao unahitaji jumla ya dola milioni 120, umefadhiliwa nus utu nab ado unahitaji dola zingine milioni 60 ili kumfikia kila muhitaji.