Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chombo cha kuepusha ukwepaji sheria Maziwa Makuu kuzinduliwa Nairobi

Chombo cha kuepusha ukwepaji sheria Maziwa Makuu kuzinduliwa Nairobi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limejulishwa kuwa mtandao wa ushirikiano wa mahakama kwenye ukanda wa maziwa makuu barani Afrika utazinduliwa tarehe 10 mwezi huu mjini Nairobi Kenya. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa ya Flora)

Baraza hilo limekutana leo New York, Marekani kupokea ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu utekelezaji wa mkataba wa amani, ulinzi, usalama na ushirikiano kwa ajii ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na ukanda huo.

Wakati akiwasilisha ripoti hiyo, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kwenye ukanda huo Said Djinnit amesema licha ya changamoto huko Mashariki mwa DRC, nchi wanachama wa mkataba huo wanasonga kutekeleza na mafanikio ni pamoja na kuanzishwa kwa mtandao huo wa ushirikiano baina ya mahakama akisema..

(Sauti ya Djinnit)

“Mtandao huo ukijumuisha wawakilishi wa nchi wanachama wa ICGLR , ukisaidiwa na wadau wa kimataifa na kikanda, utasaidia kukabiliana na ukwepaji sheria kwenye maziwa makuu kwa kujenga kuaminiana baina ya nchi wanachama na kuendeleza utekelezaji sahihi wa ahadi za ushirikiano wa mahakama.”

Ripoti ya leo imegusa kipindi cha kuanzia tarehe Tisa mwezi Machi mwaka huu hadi tarehe 20 mwezi Septemba ambapo Djinnit amepongeza nchi wanachama wa mkataba huo kuendelea kuutekeleza licha ya changamoto, akisema..

“Kumekuwepo na jitihada mpya za kushughulikia tatizo hilo lililodumu. Ushirikiano umeimarishwa kati ya jeshi la serikali, FARDC na lile la MONUSCO kwenye operesheni za pamoja dhidi ya vikundi vilivyojihami mashariki mwa DRC ikiwemo vile vya FDLR na ADF.”