Raia wana jukumu kubwa kuimarisha usalama Ituri- MONUSCO

2 Novemba 2016

Waasi wa wa FRPI na wale wa Mai Mai Simba huko Ituri, jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC waache vitendo vyao vya unyanyasaji dhidi ya raia, amesema kamanda mkuu wa vikosi vya ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko DRC, MONUSCO Luteni Jenerali Derrick Mgwebi. Rosemary Musumba na ripoti kamili.

(Taarifa ya Rosemary)

Kamanda Mgwebi alikuwa ziarani jimboni Ituri kwa siku nne ambapo alikutana na viongozi wa kisiasa, vikundi vya kiraia na wananchi, wakati huu ambapo vikundi vilivyojihami vimekuwa vikinyanyasa raia kwa tarkibani miezi miwili.

Ametolea mfano vitongoji vya Mambasa na Irumu ambako waasi wa Mai Mai Simba na FRPI wanatesa raia na hata kupora mali za wananchi.

Ametoa wito kwa mashirika ya kiraia kwenye maeneo hayo kushiriki katika kampeni ya kuhamasisha vikundi vilivyojihami kusalimisha silaha, akiongeza kuwa ingawa jeshi la serikali FARDC na MONUSCO wanawajibika kwa usalama, bado jukumu kubwa linasalia kwa raia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter