Ufaransa, Uingereza zimeshindwa kutekeleza makataba wa haki za watoto-OHCHR
Umoja wa Mataifa umesema Ufaransa na Uingereza zimeshindwa kutekeleza wajibu wao wa makataba wa haki za watoto kutokana na jinsi walivyohudumia kundi hilo wakati wa kufungwa kwa kambi ya muda wakimbizi muda ya Calais.
Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa OHCHR, kamati inayosimamia namna nchi zilizosaini mkataba wa hakiza watoto zinavyoutekeleza, imetaka nchi hizo mbili kushughulikia mara moja watoto walioko peke yakeo bila wazazi au walezi na ambao hawana malazi.
Watoto hao wameleazimishwa kulala katika makontena yasiyotumika au nje baada ya kufungwa kwa kambi hiyo ya muda.
OHCHR imesema kuwa matukio ya juma lililopita imeonyesha wazi kuwa licha ya hadi za Ufaransa na Uingereza kuwa watoto wangekuwa kipaumbeel chao, masuala ya kisiasa yametupilia mbali ahadi hizo.
Kutokukubaliana baina ya nchi hizo kuhusu nani awajibike kwa watoto hao kumesababisah uvunjifu wa haki za kundi hilo ambapo mamia yao wameishi katika mazingira yasiyo ya kibinadamu, hawana malazi, chakula, huduma za afya, msaada wa kisaikolijia na wengine wamekumbana na wasafirishaji haramu.