"Biashara kama kawaida si chaguo" kwa wakulima: FAO

7 Novemba 2016

Rob Vos ambaye ni mkurugenzi wa maendeleo ya uchumi wa kilimo katika shirika la chakula na kilimo FAO amesema kuwa "Biashara kama kawaida si chaguo" kwa ajili ya wakulima kote duniani,

Akiongezea kuwa mabadiliko ya hali ya tabia nchi yanaathiri tija na maisha ya wakulima, hasa katika nchi zinazoendelea na shirika hilo limetoa onyo kwamba takriban watu milioni 120 wanaweza kutumbukia katika umaskini ikiwa watashindwa kukabiliana na hali hii mpya kufikia mwaka wa 2030.

Kuanzia leo Jumatatu 7 Novemba jumuiya ya kimataifa inaanza mkutano wa 22 wa mabadiliko ya tabianchi au (COP22) mjini Marrakesh Morocco kujadili hatua zilizochukuliwa kwenye ahadi ya kihistoria ya mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya tabianchi.

Bwana Vos alipohojiwa na idhaa hii kwa nini kilimo ni kiini cha mabadiliko ya tabia nchi amesema…

(Sauti ya Vos)

"Kilimo tayari kinaathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na kubwa zaidi ukame, upungufu wa mvua ni kawaida. Inahisiwa kilimo pia kinaleta karibu asilimia 20% ya hewa chafuzi. Hali hii inabadilisha kilimo na kwamba biashara kama kawaida si chaguo kwa wakulima, kuna uharibifu na matumizi mabaya ya ardhi. Kuna haja ya kukarabati uwezo wa dunia kama upandaji miti na matumizi endelevu ya ardhi".

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter