Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zahma za Juba, kamanda UNMISS kubadilishwa

Zahma za Juba, kamanda UNMISS kubadilishwa

Kufuatia kuwasilishwa kwa ripoti ya uchunguzi wa zahma huko Juba, Sudan Kusini iliyobainisha kuwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS haukuwajibika ipasavyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza baadhi ya mapendekezo na hatua alizochukua.

Akizungumza na wanahabari, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric ametaja hatua hizo kuwa ni pamoja na..

(Sauti ya Dujarric)

“Ametaka kubadilishwa kwa kamanda wa vikosi, na hiyo ni moja ya mapendekezo ambayo yatatekelezwa mara moja, na mengine yatafuata.”

Kamanda huyo mkuu wa UNMISS Luteni Jenerali Johnson Mogoa Kimani Ondieki kutoka Kenya alishika wadhifa huo kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Katibu Mkuu alipokea ripoti  hiyo hii leo kutoka kwa kiongozi wa jopo la uchunguzi Patrick Cammaert.