Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tupeni ruhusa salama ya kupeleka msaada:WFP

Tupeni ruhusa salama ya kupeleka msaada:WFP

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP kwa mara ya kwanza limeweza kutoa msaada wa chakula kwa wakimbizi wa ndani  9,000 waliosambaratishwa na vita katika kata ya Lanya, Sudan Kusini huku wengine wengi bado wakinasa kwenye maeneo yasiyofikika.Taarifa kamili na RosemaMary Musumba

(Taarifa ya Rosemary)

Akizungumza na Redio Miraya nchini humo, Afisa wa WFP George Fominyen amesema wakimbizi hao ambao wanakimbilia maeneo mengine ya mbali na vichakani kujificha hawajapata chakula miezi na miezi na ni maeneo ambayo misaada muhimu haiwezi kuwafikia.

Amesema ikiwa shirika hilo halijajiandaa kusafirisha na kuhifadhi chakula katika maeneo hayo kabla ya msimu wa ukame unaobisha hodi na kufuatiwa na mvua kali,  basi hali hii itazidi kuwa mbaya zaidi, na hivyo akatoa wito...

(Sauti ya Fominyen)

"Tunatoa wito kwa wahusika wote katika mzozo, kuturuhusu kupeleka chakula katika maeneo ambayo watu watakuwa na faraja na usalama wa kupokea msaada, kwani ni muhimu kusaidia watu, lakini si kwa njia itakayohatarisha maisha yao".